Ijumaa 15 Mei 2026 - 19:47
Ujumbe wa Kiongozi wa Mapinduzi kutokana na mnasaba wa Siku ya Kuilinda Lugha ya Kifarsi na Kumuenzi Ferdowsi

Hawza/ Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu katika ujumbe wake kutokana na mnasaba wa Siku ya Kuilinda Lugha ya Kifarsi na Kumuenzi Ferdowsi alisisitiza kwamba: Taifa pendwa la Iran katika “Ulinzi Mtakatifu wa Tatu” pia, kama ilivyokuwa katika vita viwili vya awali vya kulazimishwa, limethibitisha kwamba simulizi za kishujaa za Ferdowsi zilikuwa ni uhalisia wa maisha na tabia yao ya kishujaa, na kwamba mafundisho ya kujenga utu, ya kishujaa, na ya Qur’ani yaliyomo ndani ya Shahnameh huwafanya makabila na matabaka yote ya Iran kuwa na mshikamano, kuandamana pamoja na kuwa kitu kimoja katika kulinda utambulisho wao, asili yao na uhuru wao, na katika kupambana dhidi ya wavamizi “wanaofanana na Zahhak”.

Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Habari la Hawza, ujumbe wa Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, umetolewa kutokana na mnasaba wa tarehe 25 Ordibehesht HS, Siku ya Kulinda Lugha ya Kifarsi na Kumuenzi Hakim Abul-Qasim Ferdowsi.

Matini ya ujumbe huo ni kama ifuatavyo:

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema, Mwenye Kurehemu.

Lugha ya Kifarsi, mbali na kuwa chombo cha mazungumzo na maandishi, ni mfumo wa utambuzi na kiungo cha kuunganisha fikra pamoja na mipaka ya utambulisho wa Wairani. Lugha na fasihi ya Kifarsi ni miongoni mwa nyenzo kubwa kabisa za kueneza utamaduni na ustaarabu tajiri wa Iran ya Kiislamu katika upeo wa dunia. Nausia wa kiongozi wetu mwenye hekima na shahidi — Mwenyezi Mungu autukuze cheo chake kitukufu — kuhusu kuifanya lugha ya Kifarsi iwe yenye nguvu, ni taa ya kuongoza katika kuimarika kwa “ustaarabu wa Kiirani”.

Taifa pendwa la Iran katika “Ulinzi Mtakatifu wa Tatu” pia, kama ilivyokuwa katika vita viwili vya awali vya kulazimishwa, limethibitisha kwamba; simulizi za kishujaa kimfano za Ferdowsi zilikuwa ni uhalisia wa maisha na tabia yao ya kishujaa, na kwamba mafundisho ya kujenga utu, ya kishujaa, na ya Qur’ani yaliyomo ndani ya Shahnameh huyafanya makabila na matabaka yote ya Iran kuwa na mshikamano, kuandamana pamoja na kuwa kitu kimoja katika kulinda utambulisho wao, asili yao na uhuru wao, na katika kupambana dhidi ya wavamizi “wanaofanana na Zahhak”. Hamasa hii ya uwepo, ya kujihami na ya ushindi, inaweka jukumu kubwa juu ya mabega ya watu wa tamaduni, fasihi na sanaa ili wasimame kama alivyoinuka Ferdowsi na wakafanikisha utume wa wasanii sambamba na utume wa wananchi; wachanganye fikra, kalamu na lugha pamoja na sanaa, na waifanye simulizi ya mwamko mkubwa wa taifa hili ibaki milele katika historia.

Kwa upande mwingine, kusimama kishujaa na ushindi wa kujivunia mbele ya uvamizi wa watu wenye tabia za kishetani na mashetani wa dunia, kumeliandaa taifa zaidi kwa ajili ya kulinda uhuru wa ustaarabu wake na kukabiliana na uvamizi wa lugha, utamaduni na mtindo wa maisha wa Kimarekani; ili kwa ubunifu na uanzilishi wa wanaharakati wa uga wa utamaduni, katika njia ya kuhakikisha ulinzi wa lugha na wa fikra pamoja na kukuza na kustawisha watoto na vijana, lipitie kwa uthabiti mkubwa zaidi hatua zilizobakia mpaka kufikia ushindi wa mwisho, kwa msaada wa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei
25/Ordibehesht/1405 - 15 May 2026

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha